Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, wahanga na waathirika wa tukio la ajali ya barabarani ya mabasi ya kampuni ya City Boy yaliyogongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 29, jana katika kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vilivyokuwa katika eneo la tukio zinadai kuwa mabasi hayo ambayo moja lilikuwa likitoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama na jingine likitoka Kahama kwenda Dar es Salaam, vimeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kufanya mzaha kwa kusalimiana huku wakiyumbisha magari .

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi usio na tahadhari kati ya mabasi hayo mawili.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Magufuli ameeleza kupokea kwa mshtuko taarifa hizo zilizosababisha vifo vya Watanzania.

“Namuomba Mwenyezi Mungu awape uvumilivu na ustahimilivu wanafamilia wote waliopoteza jamaa zao, sote tuwaombee marehemu wapumzishwe mahali pema peponi, amina,” alisema Rais Magufuli.

Lowassa adaiwa kujipanga kung’oka Chadema..!
Kitwanga afunguka kuhusu kutumbuliwa na JPM, Sakata la Lugumi