Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa hadi sasa viongozi wengi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, mawaziri na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kwamba Dar es Salaam amebaki yeye tu.
“Nimebaki mimi tu hapa. Nimepanga kabla mwaka huu haujamalizika nitahamia Dodoma, nilitaka nisihamie huko nikawaacha ndugu zangu wanaowakilisha nchi zao hapa Dar es Salaam, ndiyo mana nikahakikisha mnapata hati.
Aidha, amesema kuwa tayari viongozi wote na watumishi zaidi ya 6,000 wameshahamia huko ambapo pia amewatoa hofu mabalozi hao na wawakilishi wa kimataifa kuhusu usalama jijini humo.
-
Jokate: Uvumilivu ndio ulionifikisha hapa nilipo
-
Video: Haji Manara afunguka kuhusu Jerry Muro kuteuliwa Ukuu wa Wilaya
-
RC Mghwira alitaka Jeshi la Polisi kujitathmini
Hata hivyo, ameongeza kuwa amemuagiza kuanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato ili ndege zinazotua jijini Dar es salaam ziwe zinatua jijini Dodoma.