Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amesema ushindi wa CCM wa ubunge na madiwani katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika juzi nchini ni ishara ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi ujao kutokana na wananchi kuonyesha imani kwake na Serikali yake.
Rais Magufuli amesema ushindi huo ni kipimo cha utendaji wake kwa wananchi na hivyo umemuongezea ari ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wake bila ya kujali changamoto mbalimbali zilizopo.
“CCM Oyee! Mnaonaje ushindi wa CCM? Hii inadhihirisha ni namna gani wananchi walivyo na imani na mimi na Serikali yangu. Tumeshinda ushindi kwa kishindo katika kata na Jimbo, wenyewe mmeshuhudia namna tulivyowapiga. Amesema Rais Magufuli.
Mbali ya kushinda kiti cha ubunge cha Dimani visiwani Zanzibar, CCM imeshinda kata 18 kati ya kata 19 zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani juzi kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kufa kwa waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo na kufutwa kwa matokeo kwa amri ya mahakama.
Kata ambazo CCM imeshinda ni Nyarenanyuki (Arumeru, Arusha), Isegehe (Kahama, Shinyanga), Nkome (Geita), Kiwanja cha Ndege (Manispaa Morogoro), Lembeni (Mwanga, Kilimanjaro), Ihumwa (Dodoma), Matevez (Meru, Arusha), Kimwani (Muleba, Kagera), Igombavanu (Iringa), Kijichi (Mbagala, Dar es Salaam), Ng’hambi (Dodoma), Kinampundu (Singida), Kasansa (Katavi), Malya na Kahumulo (Mwanza), Mkoma (Mara), Misugusugu (Kibaha, Pwani).
Aidha, CCM imeshindwa katika Kata ya Duru mkoani Manyara, ambako mgombea wa Chadema, Ali Shaaban ameibuka mshindi. Kwa upande wao, baadhi ya wasomi wamesema kwamba chama cha mapinduzi kimeshinda kutokana na kutekeleza ahadi za kuondoa kero za wananchi.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Francis Michael amesema kwamba wananchi wa kada za chini wanaiamini CCM kwa sasa hivi kwa kuwa Rais John Magufuli amejikita kushughulikia masuala yanayowakera.

Serikali yatoa onyo kwa wanaotangaza baa la njaa
AFCON 2017: Algeria Yatupwa Nje