Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajia kulihutubia Bunge la 12 Novemba 13, kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za utendaji wa viongozi waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, alipokuwa akiahirisha kikao cha pili cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 12.
“Naomba wabunge wote muwepo Bungeni siku hiyo Rais atalihutubia bunge lakini kupitia sisi atakuwa akihutubia taifa” amesema Spika Ndugai leo asubuhi wakati akiahirisha kikao cha Bunge.
Shuguli za Bunge zimeahirishwa hadi kesho Novemba 12, 2020 ambapo Bunge linatarajia kupokea jina la Waziri mkuu.