Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewapongeza mawaziri pamoja na manaibu waziri kwa kuanza kazi vizuri mara baada ya kuapishwa na kuanza kutumikia nafasi hizo.
Amesema hayo leo Dec 16, 2020 wakati akifungua kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri, cha muhula wake wa pili wa serikali ya awamu ya tano.
Kikao hicho amabcho kimehudhuriwa na na Makamu wa Rais Samia suluhu, Waziri mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, mawaziri 23 pamoja na manaibu wao.
Manaibu 21 pamoja na manaibu waziri waliohudhuria katika kikao hicho waliteuliwa Desemba 5, 2020, na kuapishwa na Rais Magufuli katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma tarehe 9 desemba mwaka huu.