Mgombea nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dokta john Magufuli ,amesema kuwa endapo chama chake kitapata nafasi ya kuongoza kwa awamu ya pili kitanedelea kutoa elimu bila malipo.
Akiwahutubia katika kampeni wanchi wa wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga amesema kuwa serikali yake itaendelea kuboresha huduma za jamii pamoja na elimu bila malipo.
” Watoto wanasoma bila ada, hata Ulaya wanalipa ada ila sisi ni Bure,tumejipanga miaka 5 ijayo kuendelea kuboresha huduma za jamii, tutatoa elimu bila malipo, kuboresha afya” amesema.
Magufuli amesema kuwa katika kuboresha elimu serikali ya CCM inatarajia kutangaza ajira zaidi ya elfu 13 za walimu wa shule za msingi na sekondari .
“Nilikuwa naongea na Maafisa Elimu, hivi karibu tunatangaza ajira za Walimu wa shule ya msingi na sekondari zaidi ya Elfu 13 ili shule zetu zipate Walimu wa kutosha, tunatoa Elimu bure sasa tunaongeza na Walimu” amesema Magufuli.