Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars’, Jamhuri Kiwelo Julio’, ameamkingia kifua kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouch kutokana na kutowaita baadhi ya nyota kama Feisal Salum, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kikosini mwake.
Wachezaji hao wameachwa katika kikosi ambacho kocha Amrouch amekiita kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa mwisho wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Algeria itayopigwa Septemba 7, mwaka huu.
Julio amesema kuwa: Kocha anataka kuhakikisha kuwa timu inafuzu hivyo kuwaacha wachezaji kama Feisal Salum, Kapombe na Zimbwe ni kutokana na sababu ambazo yeye mwenyewe anazifahamu.
Mimi naamini kocha anazo sababu ambazo zimewafanya asiwaite kwani ukiangalia mchezaji kama Feisal kutokana na kiwango ambacho amekionyesha kwa sasa, pengine hakikumshawishi kocha kukumuita na kuwapa nafasi wachezaji wengine.
“Ukija kwa upunde wa Zimbwe na Kapombe hawa ni wachezaji ambao wanecheza kwa muda mrefu katika kikosi cha timu ya taifa hivyo kuachwa kwao ni kawaida kwa kuwa imetokea duniani kote, hivyo tumpe mwalimu beshima yake naamini kuna kitu amekiona.”