Meneja wa Kikosi cha Liverpool Jurgen Klopp, amesisitiza kuwa, wana nafasi kubwa ya kuwapiga vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu ya England Arsenal, keshokutwa Jumapili (April 07).

Liverpool inatarajia kuikaribisha Arsenal katika Uwanja wa Anfield ikiwa katika haliambaya msimu huu, ikilinganishwa na misimu kadhaa iliyopita ambapo The Reds katika kipindi kama hiki walikua wanawani nafasi za juu ama ubingwa wa England.

Meneja huyo kutokanchini Ujerumani amesema hayo, baada ya kushuhudia kikosi chake kikilazimishwa sare mbele ya Chelsea katika mchezo uliopigwa jijini London katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Arsenal ambao msimu huu wameonesha kuwa tofauti, watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanashinda mchezo huo, ili kuendelea na harakati zao wa kuufukuzia ubingwa wa England, ambao kwa mara ya mwisho waliutwaa msimu wa 2003/04, chini ya Arsene Wenger.

Liverpool katika michezo miwili iliyopita, imefanikiwa kupata alama moja pekee mbele Chelsea, huku ikipoteza dhidi ya Manchester City kwa kufungwa 4-1.

Kocha Klopp anaamini kuwa kiwango walichoonesha wachezaji wake dhidi ya Chelsea iliyokua nyumbani Stamford Bridge kitaendelea kuwa bora watakapocheza dhidi ya Arsenal katika Uwnaja wao wa Anfield keshokutwa Jumapili.

Klopp ambaye aliipa Liverpool ubingwa wa ligi msimu wa 2019/20 baada ya kupita takribani miaka 30, amesema: “Arsenal wapo juu na wanacheza soka safi, lakini naweza kucheza na kuwa bora zaidi yao.”

“Mchezo ujao ni dhidi ya Arsenal. Sijui kabisa Arsenal walikuwa nafasi ipi msimu uliopita, ila kwa sasa wapo juu na wapo vizuri, wanacheza soka zuri ambalo linavutia kuangalia.”

“Lakini sasa tutakuwa nyumbani na tukiwa nyumbani tuna rekodi zetu ndiyo maana tumewekeza nguvu katika mchezo huu. Anfield inatusubiri sisi na sisi tunataka kuonesha kitu.”

“Tuna michezo 10 ya kucheza na ujayo ni dhidi ya Arsenal, kwa sasa tunawaangalia hawa kwanza.” “Najua kuna ugumu lakini ni lazima tupambane kushinda huu mchezo tofauti na hapo watazidi kuwa juu, tunataka kubadili mambo na si vinginevyo.”

Serikali yafikiria kuharamisha ajira za kigeni sekta ya Afya
William Saliba bado majanga Arsenal