Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kuwa tayari kutoa ofa ya kumsajili kwa mkopo Mason Greenwood kutoka Manchester United.

Mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, bado haujulikani na tetesi zinaendelea kuzagaa kuhusu ofa kutoka nje ya nchi.

Anaendelea kufungiwa na klabu huku wakifanya uchunguzi wa ndani kuhusu tuhuma za ubakaji zinazomkabili.

Greenwood alikamatwa Januari 2022 baada ya tuhuma za kujaribu kubaka na kushambulia, lakini mashtaka dhidi yake yalitupiliwa mbali Februari 2023.

Bado hajarejea kufanya mazoezi na klabu hiyo na inadhaniwa kuwa anaweza kufanya hivyo mwanzoni mwa msimu ujao.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa Juventus wamepiga hatua kwenye kambi ya Greenwood juu ya uwezekano wa kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu.

Mchezaji mwenzake wa zamani, Paul Pogba, yumo kwenye kikosi hicho na inatumainiwa kuwa anaweza kubadili mambo kwa upande wa Serie A. Pia AC Milan na Roma wanadaiwa ku- vutiwa naye.

Tume utawala bora yaingilia kati mkanganyiko ajali ya Naibu Waziri
Polisi wamuaga rasmi IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro