Serikali ya Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, imewasilisha malalamiko mapya ikidai kuendelea kuwa na janga la kibinadamu linalosababishwa na uchokozi wa Taifa la Rwanda inayoongozwa na Rais Paul Kagame ndani ya ardhi yake.
Waziri wa Mawasiliano, Patrick Muyaya na Waziri wa Sheria, DRC Rose Mutombo wote wa DRC waliwasilisha kesi yao dhidi ya Serikali ya Kigali katika mkutano na Hanahabari katika mji mkuu na Nchi hiyo, DRC, wakidai Rwanda imekuwa imekuwa ikiwaunga mkono waasi wa M23.
Kikosi hicho, kimeteka maeneo mengi ya eneo la Kivu Kaskazini kwenye mpaka wa nchi hizo mbili, tangu kuchukua tena silaha mwishoni mwa 2021 baada ya kukaa kimya kwa miaka mingi na tuhuma hizo zimekuwa zikikanushwa na Taifa la Rwanda mara kwa mara.
Hata hivyo, Muyaya alidai ana ushahidi usioweza kukanushwa wa vitendo vya uhalifu vinavyoendeshwa na jeshi la Rwanda na wafuasi wake wa M23, huku akidai kuwa mzozo huo umewalazimu zaidi ya watu milioni 2.3 kukimbia makazi yao na kuacha mamia ya shule yakiharibiwa.