Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.

Kairuki amesema umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuhamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.

“Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Amesema Kairuki.

Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na  litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.

Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma lakini.

 

TCRA yawatahadharisha wananchi kuhusu utapeli wa simu
Tanzania na Uturuki zasaini mikataba tisa ya maendeleo