Maafisa waandamizi wa mashirika ya upelelezi nchini Marekani wako katika kikao cha mahojiano kwa ajili ya tathmini ya vyombo vyao kwamba Urusi ilifanya udukuzi katika uchaguzi wa rais na kumsaidia Donald Trump kushinda.
Kikao cha mahojiano cha kamati ya huduma za majeshi ya taifa kuhusu kitisho mtandaoni leo Alhamis kimekuja siku moja kabla ya rais mteule wa Marekani Donald Trump kupewa taarifa na wakurugenzi wa mashirika ya ujasusi CIA na lile la uchunguzi wa makosa ya jinai FBI, pamoja na mkurugenzi wa usalama wa taifa, kuhusiana na uchunguzi juu ya madai ya udukuzi.
Lakini msemaji wa Ikulu ya Marekani ya White House, Josh Earnest amesema tathmini iliyotolewa kwa pamoja na vyombo vya upelelezi inaonesha wazi kuwa Urusi ilikuwa ikiingilia shughuli za uchaguzi nchini Marekani.
Tarifa hiyo ambayo ilitolewa na vyombo vya upelelezi Oktoba mwaka 2016 kabla ya uchaguzi inaweka wazi kwamba Urusi ilikuwa inaingilia kati katika uchaguzi woete na kuwalikisha mtazamo wa pamoja wa mashirika 17 tofauti ya upelelezi. Hii si kawaida ya vyombo hivi kufanya kazi. Hali ya mawazo yanayolingana, hususan hali ikiwa ya mvutano, ni suala la kutafakari. Uamuzi wa vyombo vya upelelezi, sio tu kufikia hitimisho lakini kuiweka wazi ripoti yao, ni jambo kubwa na nafikiri inaakisi kina cha hali yao ya kuamini tathmini yao.”
Shutuma za Urusi kuingilia katika uchaguzi wa mwaka 2016 kwa kudukua kurasa za barua pepe za chama cha Democratic kilipelekea Rais Barack Obama alilipize kwa kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi mwishoni mwa mwezi Desemba kwa kuchukua hatua ya kuweka vikwazo vinavyolenga mashirika ya ujasusi ya Urusi, lile la GRU na FSB, ambayo Marekani ilisema yanahusika. GRU ni shirika la Urusi linaloshughulika na masuala ya ujasusi wa kijeshi. Lile la FSB ni mrithi wa shirika la wakati wa enzi za Umoja wa Kisovieti la KGB.