Makamu wa Rais mteule wa Marekani Mike Pence, amesema kuwa mchakato wa kuifuta sheria ya afya iliyoanzishwa na Obama utaanza siku ya kwanza Donald Trump atakapoingia madarakani.

Ameyasema hayo kwenye mkutano na wanachama wa Republican na viongozi katika bunge la congress,Pence amesema Rais mteule alikuwa anashughulikia sheria mahususi zinazohusika ili kuruhusu mabadiliko kuelekea katika mfumo mpya wa sheria za afya.

Kwa upande wake Trump amesema kuwa wanachama wa Republican wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanachama wa Democratic wanalaumiwa kwa kile alichokitaja kuwa ni Maafa ya sheria ya afya yaliyoanzishwa na Barack Obama.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha Democratic katika bunge Chuck Schumer amesema chochote kilichotokea ni jukumu la Republican jambo ambalo ni wazi na rahisi.

 

Kamati ya bunge la Marekani yaanza uchunguzi dhidi ya Urusi
Mpinga: Hakuna trafiki anayelipwa kukamata magari