Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imepitisha mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Bajeti hiyo, imepitishwa na kikao hicho cha kamati kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Fatuma Toufiq ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako aliiongoza Menejimenti kuwasilisha mpango na bajeti ya ofisi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatuma Toufiq akieleza jambo wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatuma Toufiq wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, kilichofanyika Bungeni, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na menejimenti ya ofisi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma.

BAKWATA waandamana kupinga ukatili kijinsia, ndoa za utotoni
Tanzania, Marekani, kuendeleza uhusiano Kidiplomasia