Licha ya kuwa sehemu ya msafara wa kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania bara Simba SC huko nchini Morocco, Kocha Msaidizi Suleyman Matola bado yupo masomoni.

Matola anasomea leseni B ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’, na tayari ameshamaliza hatua ya awali ya darasani na sasa amerudi kufanya kazi kwa vitendo “field” kwenye timu ya Simba SC.

Kocha huyo mzawa anaatarajia kutumia muda wa maandalizi ya kikosi cha Simba SC huko nchini Morocco, kama sehemu ya kutimiza majukumu ya masomo yake ya miezi mitatu.

Hata hivyo uwepo wa Kocha Mkuu Didier Gomes kambini hapo, utamsaidizi Matola kutimiza sehemu ya majumu yake kimasomo, ili kufikia lengo la kukamilisha Program maalum aliyopewa darasani.

kikosi cha Simba SC kiliwasili mjini Casablanca nchini Morocco, tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa, itakayoanza rasmi mwezi Septemba.

Simba SC inatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu, kuendelea na maandalizi ya msimu ujao, huku ikitarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika simu maalum ‘SIMBA DAY’ mnamo Agosti 28.

Aina ya ukataji nywele yamponza An San
Abdul Basit Khalid anukia kwa Mabingwa wa Tanzania Bara