Kambi kadhaa za kijeshi nchini Burundi jana zilishambuliwa usiku kucha katika maeneo kadhaa ya jiji la Bujumbura.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mshauri wa rais Pierre Nkurunzinza, Willy Nyamitwe, mashambulizi hayo yalifanywa na wapinzani wa serikali kwa lengo la kuwafungulia wafungwa walioshikiliwa katika kambi hizo.

Nyamitwe alieleza kuwa mpango wa washambuliaji hao haukufanikiwa baada ya maafisa wa ulinzi wa jeshi la serikali ya Burundi kuwatimua wote.

Kufuatia tukio hilo, jeshi la Burundi limefanya msako mkali na kukamata silaha kadhaa zilizokuwa mikononi mwa raia.

Mashambulizi dhidi ya jeshi la Burundi yamekuwa yakitekelezwa mara kadhaa nchini humo tangu rais Nkurunzinza alipoamua kugombea urais kwa awamu ya tatu na kukabiliwa na jaribio la Mapinduzi ya kijeshi.

Serikali nchini humo imewataka raia wote wanaomiliki silaha kujisalimisha na kuwataja watu wengine wanaomiliki silaha hizo vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

chanzo: BBC

Rais Wa TFF Ampongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo
Madiwani Wa Ukawa Na CCM Washikana Mashati, Polisi Waingilia Kati