Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amewataka Wananchi wa Mkoa wa Katavi kuachana na imani potofu za kishirikina, ambazo zimekuwa zikififisha juhudi za kupambana na umaskini, ili kukuza maendeleo na ustawi wa watu.

Chongolo ameyasema hayo wakati akizungumza na wana CCM na wananchi katika eneo la Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Katavi, Mpanda Mjini, baada ya kuwasili mkoani humo kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, kuhamasisha uhai wa Chama mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi.

“Nimeambiwa huku kuna kamchape , hawa jamaa mnawapa nguvu kubwa, mnawapa kichwa, mnawapa fursa ya kufanya mambo yanayokiuka sheria za nchi, imani hizo za kuamini ushirikina ni umasikini na ukitaka kujifunza angalia watu wanaoamini katika ushirikina uone maisha yao. Wanaamini katika ndoto ambazo kutekelezeka kwake ni ngumu,” alisema Chongolo.

Aidha aliongeza kuwa, “naombeni sana achaneni na kuendekeza mambo yanayoleta taaswira ya umasikini. Mkoa wa Katavi ni mkubwa na mmeshajenga historia kubwa’
Ndungu Chongolo amesema haiwezekani mpaka leo Mkoa wa Katavi kuendekeza ushirikina kama daraja la kufanikiwa katika mambo yao , hivyo ni lazima watoke katika kufikiri mambo kirahisi.”

Chongolo ameongeza kuwa, maendeleo hayapatikani kwa ndumba, kwa kupuliza, kwa kuagua , kupiga ramli na kutengeneza mambo rahisi bali maendeleo ni mambo yanayotaka kufuata utaratibu wa kanuni za maisha.

“Ukiona watu wa namna hiyo wewe usipate shida angalia maisha yao, mtu anaweza kuwa na ng’ombe 1000 lakini anakula nyama nusu kilo kwa wiki, sababu ya masharti.Achaneni na maisha hayo , afadhali uwe na ng’ombe 10 lakini uwe na uhuru wa kula nyam ni afadhali uwe na shamba heka tatu lakini uwe na uhuru wa kula mchele wako, achaneni na mila potofu , mila potofu zinawatenganisha,” amesema.

Alexis Mac Allister hatarini kufungiwa England
Robertinho: Kikubwa tumefuzu, mengine yanafuata