Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation – ZMBF, Mariam Mwinyi amesema kampeni ya Afya Bora Maisha Bora imelenga kuunga mkono juhudi za Serikali kufikia huduma za afya bora Zanzibar.
Mama Mariam ameyasema hayo Septemba 30, 2023 baada ya matembezi ya “Mariam Mwinyi Walkathon” na kuzindua program maalum inayojulikana kwa jina la “Afya Bora Maisha Bora” inayojumuisha uwepo wa kambi ya matibabu bure kwa wananchi Zanzibar iliyoandaliwa na Taasisi ya ZMBF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Afya check.
Amesema, kipaumbele kimojawapo cha Serikali ni kuimarisha Afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za masafa, kuwafuata wananchi walipo.Vilevile kampeni hii itasaidia kuwajengea wananchi tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu pale ugonjwa unapogundulika mapema.
Hata hivyo, ameongeza kuwa katika ufikiajinwa utoaji wa huduma bora pia watawapatia Wananchi elimu ya afya, kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na kupata matibabu hadi ngazi ya rufaa kwa hospitali zote nchini.