Sakata la kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini (Makinikia) ambalo lilipelekea kuundwa kwa tume ya uchunguzi wa  makontena yaliyozuiliwa katika bandari ya Dar es salaam limechukua sura mpya mara baada ya Kampuni ya Acacia kukubali kulipa mirahaba iliyowekwa katika sheria mpya ya madini.

Tume ya uchunguzi iliyokuwa imeundwa na Rais Dkt. John Magufuli ilipendekeza kuwa lazima kuwepo na marekebisho katika sheria ya madini huku ikiishauri Serikali kutoruhusu mchanga huo wa madini mpaka itakapolipwa mirahaba.

Katika sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katika sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirahaba ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali ikiwa ni pamoja na asilimia 1 kwaajili ya kusafirisha nje.

Aidha, katika bunge la bajeti lililomalizika hivi karibuni liliongezewa muda kwaajili ya kutoa mapendekezo ya marekebisho sheria ya madini ambayo ilikuwa na mapungufu katika baadhi ya vifungu.

Hata hivyo, hivi karibuni Kampuni ya Acacia ilifungua kesi ya usuluhishi kati yake na Serikali kuhusu mgogoro unaohusiha usafirishaji wa mchanga wa madini (Makinikia) kwenda nchi za nje.

 

TCRA yazikomelea msumari wa moto Kampuni za simu
Mwakyembe: Serikali hairidhishwi na kampuni ya ubia kati ya TBC na Star Times