Waziri wa Habari, Dkt Harrison Mwakyembe amezungumza na vyombo vya habari TBC kuhusu suala la mkataba wa TBC na Kampuni ya kuuza Ving’amuzi ya Star Times.

Mwakyembe amelalamikia huduma zinazotolewa na ving’amuzi vya Startimes na kusema kuwa serikali hairidhishwi na kampuni ya ubia kati ya TBC na Star Times kwani huzalisha hasara kila mwaka.

Hivyo Waziri Mwakyembe leo amekutana na mwenyekiti wa Star Times, Pang kujadili mkataba huo ili kufanya uamuzi mwezi huu.

Ambapo Mwakyembe ameamua kuunda  timu ya wataalamu kufanya kazi kwa siku saba na kutoa mrejesho kamili utaowaongoza kufanya maamuzi kama kuendelea au kuboresha ubia huo baina yao.

Aidha mwenyekiti Star Times amemshukuru Rais Magufuli kwa nia ya kutaka mkataba uwe wa mafanikio zaidi na ameahidi kurekebisha kasoro zozote zilizojitokeza.

 

Kampuni ya Acacia yakubali kulipa mirahaba iliyowekwa katika sheria mpya
Real Madrid kujaribu mara ya mwisho, yatenga dau nono