Kampuni ya Sukari ya Kilombero, imefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha cha Uanagenzi na Mafunzo (Apprenticeship and Internship), huku ikishika nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content).
Mbali na kunyakua tuzo hizo, Pia Kampuni hiyo imepokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla ya utoaji wa tuzo hizo zitolewazo na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Desemba 2, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdory Mpango (kulia) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Cleopatra Nasari, Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (katikati) kwa kudhamini hafla ya Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Desemba 2, 2022. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu (kulia), Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (kushoto) Anthony Rweyemamu baada ya Kampuni kushinda nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City tarehe 02 Desemba 2022 ambapo kampuni ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Anthony Rweyemamu Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero akipokea tuzo ya mshindi wa katika kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika tarehe 02 Desemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City ambapo kampuni pia ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited wakiwa katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Desemba 2, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City. Kampuni hiyo ilitajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo, na Mshindi wa pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masuala ya Biashara- Bruno Daniel , Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo – Cleopatra Nasari, Meneja wa Maghala Dsm/Morogoro Anthony Rweyemamu na Mtafiti wa Masoko Lenin Rugaimukamu.