Watu tisa wamefariki kutokana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa nchini Afrika Kusini, huku wengine wakijeruhiwa wakati watu hao walipokuwa wakishiriki ibada jijini Johannesburg.

Kitengo cha kukabiliana na majanga nchini humo, kimesema kundi la waumini 33 walikuwa wamekusanyika kanisani katika eneo la ukingo la mto Jukskei kabla ya mkasa huo hapo jana Jumapili Desemba 4, 2022.

Hali ilivyo katika jiji la Johannesburg. Picha ya Freight News.

Aidha, vikosi vya ukoaji na Jeshi la zima moto bado vinaendelea na jitihada ya kusaka miili ambayo bado haijapatikana, huku Polisi wakisema huenda madhara zaidi yakatokea na watazidi kutoa taarifa kila mara.

Matukio ya ghafla ya kuongezeka kwa mvua na maji ni ya kawaida katika sehemu hiyo ya jiji la Johannesburg, ambapo dhoruba hupiga karibu kila usiku wakati wa majira ya joto.

Madaktari wampigia magoti Rais ili aongeze muhula wa uongozi
Mwanasiasa mkongwe aachiwa huru