Mwanasiasa maarufu wa Sudan, Wagdi Salih ameachiwa huru kutoka gerezani ikiwa ni siku moja kabla ya jeshi na muungano wa kisiasa aliokuwa sehemu yake kusaini mpango wa makubaliano.

Salih alikuwa mstari wa mbele katika kamati ya kupambana na ufisadi, ambayo ilivunjwa na majenerali walioongoza mapinduzi ya Oktoba 2021.

Mwanasiasa maarufu wa Sudan, Wagdi Salih. Picha ya Sudan Tribune.

Muungano wake ujulikanao kama Force of Freedom and Change umekiita kitendo cha kukamatwa kwake kuwa kimechochewa na hatua za kisiasa zaidi.

Aliachiwa rasmi hapo jana Jumapili Desemba 4, 2022, huku maadhi ya wafuasi wake wakimpokea na kumtia moyo juu ya mkasa uliompata.

Tisa wafariki kwa mafuriko wakati wa Ibada
Simba SC yaikaribisha Young Africans mezani