Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Makampuni ya simu nchini yanaendelea kuishi kwakuwa Watanzania wana afya na kwamba yanapaswa kuweka mikakati endelevu itakayosaidia uendelezaji wa vita dhidi ya Malaria.
Nape ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2023 ambayo Kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kila ni lazima kuweka malengo yatakayosaidia uendelezaji wa zero Malaria.
“Makampuni ya simu mnaishi kwasababu Watanzania wana Afya, naomba muweke mikakati na nitakuja kukagua, kila Kampuni ya simu weka mkakati wa kushiriki kuhakikisha Tanzania inakuwa na zero Malaria,” amesema Nape.
Amesema, mapambano dhidi ya ugonjwa huo si kazi ya Wizara ya Afya pekee, huku Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani nchini, Dkt. Zabulon Yoti akiipongeza Tanzania kwa kuwa moja kati ya mataifa manne Afrika, yaliyopunguza vifo vitikanavyo na malaria kwa asilimia 52 ikiungana na nchi za Nigeria, Niger na Congo.