Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imeandaa mtaala wa mafunzo wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani kwa watoa huduma wa ngazi za msingi ili kuwajengea uwezo wa kutoa elimu kwa jamii.

Dkt. Mollel ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma hii leo Aprili 24, 2023 na kuongeza kuwa, miongoni mwa mikakati mingine ni kuandaa vipindi mbalimbali na machapisho ya utoaji wa elimu ya afya dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo saratani.

Amesema serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali za kutoa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na ugonjwa wa saratani kupitia vipindi vya redio na televisheni, machapisho na magazeti, mitandao ya jamii na Televisheni za sehemu za kusubiria wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.

Tanzania inatarajia kutumia Shilingi 99.09 bilioni kutibu magonjwa yasiyoambukiza kwa mwaka, ikiwa gharama hiyo imeongezeka kutoka Sh35.65 bilioni mwaka 2016/2017.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 25, 2023
Rais Mwinyi aomba usafiri wa maji Pemba, Tanga