Wakati Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC ukiendelea kufanya maboresho kwenye kikosi chao, kwa kusajili wachezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania, imefahamika kuwa klabu za Kaskazini mwa Bara la Afrika zimejipanga kuwabomoa kwa kuwasajili wachezaji muhimu huko Msimbazi.
Wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mawindo dhidi ya klabu za Kaskazini mwa Bara la Afrika ni Kiungo fundi Clatous Chotta Chama kutoka Zambia, na kiungo Mshambuliaji wa Msumbiji Luis Muquissone.
Hata hivyo Kaimu Afisa habari wa klabu ya Simba SC, Ezekiel Kamwaga amethibitisha taarifa za mawindo ya wachezaji hao dhidi ya klabu za huko Kaskazini.
Kamwaga amesema kuwa wamepokea Ofa nyingi za kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Clatous Chota chama na Luis Miquissone.
Hata huvyo Kamwaga hakutaka kuweka wazi majina ya klabu zilizowasilisha ofa kwa ajili ya wachezaji hao wawili, na kusisitiza kuwa kama watazikubali ama kuzikataa klabu hizo watazitaja baadae.
Kuhusu Luis Miquissone Kujiunga na Klabu ya Al Ahly, Klabu ya Simba SC itatangaza hivi karibuni kama wameikubali ofa ya mabingwa hao wa Afrika ama wataendelea kuwa mchezaji huyo kwa msimu ujao.