Saa kadhaa baada ya Uongozi wa Young Africans kutangaza hadharani kuachana na Walinda Lango wake, Faruok Shikalo ametoa neno la Shukurani kwa Mashabiki, Wanachama, Viongozi na Wachezaji aliofanyanao kazi kwa miaka miwili klabuni hapo.

Farouk ambaye alisajiliwa mwaka 2019 akitokea Bandari FC ya nchini kwao Kenya amemaliza mkataba wake na Young Africans sambamba na mwenzake Metacha Mnata.

Mlinda Lango huyo aliyeonesha umahiri mkubwa wa kulinda lango kila alipopewa nafasi ametoa neno la shukurani kupitia kurasa zake za mitandao ha kijamii.

Farouk ameandika: “Imekua miaka miwili kamili tangia nijiunge na timu ya wananchi Yanga Sc. Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki ambao wamekua sehumu kubwa ya maisha yangu tangu nijiunge na timu hii.

Hakika mmesimama na mm katika kipindi kigumu na mmenivumilia kwa mengi na kunipa sapoti yenu na motisha ili niendele kuipambania timu.

Ningependa pia kuwashkuru viongozi wote makocha na wachezaji wote amboa nimebahatika kufanya nao kazi hapa yanga.

Bila kusahau nitoe shukrani zangu pia kwa @kabwili13 na 33_metacha ambao tumepeana competition nzuri na kujifua nao kwa miaka hii miwili ndani ya club hii pendwa @yangasc.

Kwa sasa niseme kwaherini wananchi, ila mtabakia kua ndani ya moyo wangu siku zote. #AsanteSanaTanzania”

Aucho afunguka alivyoitosa Simba SC
Kamwaga: Tumepokea ofa kutoka Kaskazini