Kiungo Mpya wa Young Africans Khalid Aucho amefunguka kwa mara ya kwanza suala la kuikacha Simba SC na kujiunga na ‘WANANCHI’.

Aucho alitambulishwa rasmi jana Jumatatu (Agosti 09) na klabu ya Young Africans, baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho huru.

Kiungo huyo amekanusha taarifa za kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba SC kama ilivyokua ikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania na kwao Uganda.

Amesema mabingwa hao wa Tanzania Bara walizungumza na wakala wake na hawakufikia muafaka, hali ambayo ilitoa mwanya wa yeye kuangalia upande wa pili.

“Simba Sc hawakuzungumza na mimi, waliizungumza na wakala wangu.” amesema Khalid Aucho.

Katika hatua nyingine Aucho amesema sababu kubwa ya kuitosa Simba SC na kusaini Young Africans ni mahaba kwa wananchi na sio pesa.

Ukonde aondolewa Young Africans
Shikalo awaaga na kuwashukuru 'WANANCHI'