Baada ya kuwepo kwa akaunti feki ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambao ulikua unatoa taarifa mbalimbali kwa jamii kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ujumla, kuanzia leo Disemba 30, 2018, Wizara imetangaza rasmi kwa jamii, akaunti halali zilizosajiliwa kwa jina la Waziri Kangi Lugola, ambazo ni.

officialkangi_lugola (Instagram)

kangi_lugola (Twitter)

Taarifa hiyo imesema kuwa taarifa zote zitakazotolewa katika kurasa za akaunti hizo zitakua sahihi.

Aidha, Wizara imewaomba Watanzania waendelee kupata taarifa zake zaidi kupitia tovuti yenye anuani; www.moha.go.tz na twitter ya Wizara kwa akaunti ya Msemaji Mambo ya Ndani.

Hata hivyo, Wizara imetoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha kwa kutumia jina la Kangi Lugola kusajili akaunti yoyote na kutoa taarifa za Waziri huyo kupitia akaunti feki hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 

 

 

Wanajeshi 8, Mgambo 14 wa Al-Shabaab wauawa Somalia
JPM amjulia hali mama yake mzazi