Washambuliaji wasiojulikana walichoma moto makazi ya kasisi mmoja wa Kikatoliki wa Nigeria kaskazini-magharibi mwa Nigeria, na kumchoma moto kasisi mmoja hadi kufa na kumpiga risasi na kumjeruhi mwingine aliyejaribu kutoroka, huku wakitikisa imani kwa mamlaka za usalama za nchi hiyo yenye wakazi wengi zaidi barani Afrika kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika.
Sababu za washambuliaji hao wenye silaha, wanaojulikana kama “majambazi” nchini humo hazikujulikana. Lakini eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi nchini Nigeria limejaa wanajihadi ambao wamekuwa wakipigania kuanzisha ukhalifa kwa takriban miaka 14.
Kaskazini mwa nchi hiyo pia kumeshuhudiwa utekaji nyara kwa ajili ya kulipa fidia na mauaji ya magenge yenye silaha hivi majuzi, huku kukiwa na hofu kubwa kwamba uchaguzi wa rais wa Februari 25 huenda usifanyike katika baadhi ya maeneo.
Kwa mujibu wa Masemaji wa Polisi, amesema majambazi hao walishindwa kufikia makazi ya Padre Isaac Achi katika kijiji cha Kafin-Koro katika jimbo la Niger mapema Jumapili na hivyo kuamua kuchoma moto nyumba yake ambapo Kasisi mwingine, aliyetambulika kama Padre Collins, alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka nyumba iliyoungua.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters lilimnukuu Gavana wa jimbo la Niger Sani. Bello akisema “Huu ni wakati wa kusikitisha. Kwa kasisi kuuawa kwa njia kama hii ina maana kwamba sisi sote hatuko salama. Magaidi hawa wameipoteza na hatua kali zinahitajika ili kukomesha mauaji haya yanayoendelea,”
Saa kadhaa baadaye, majambazi walifanya shambulio tofauti katika jimbo la Katsina kaskazini, wakimpiga risasi kasisi na kuwachukua mateka watu watano kutoka kwa nyumba ya Wakristo walipokuwa wakijiandaa kuhudhuria misa ya Jumapili katika kanisa lililo karibu.
Juni mwaka 2022, watu wenye silaha walishambulia kanisa la Kikatoliki kusini magharibi mwa Nigeria wakati wa Misa ya Jumapili, na kuua makumi ya waumini.