Takriban watu wanne wamefariki Dunia, baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha magari mawili aina ya Toyota Spacio na Lori kugongana uso kwa uso katika eneo la Kwambe Wilayani Kilosa lililopo Barabara kuu Morogoro – Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mukama amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari dogo kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Gari aina ya Spacio, iliyopata ajali na kuuwa wanne wa familia moja.

Amesema, magari yaliyohusika katika ajali hiyo Toyota Spacio lenye namba za usajili T 162 DGN lililokuwa likitokea Dodoma Kuelekea Dar es salaam na Lori lenye namba za usajili T. 654 DDN lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Amesema, waliofariki wote walikuwa kwenye gari dogo akiwemo Dereva na miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mt. Joseph iliyopo Dumila Wilayani Kilosa kwa ajili ya utambuzi, huku mashuhuda wakidai gari hilo lilikuwa limebeba watu sita.

Mgogoro wa wakimbizi, Rais Kagame arusha jiwe gizani
Nikilala kitandani asubuhi najikuta makaburini: Mwl. Nondo