Aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amefariki dunia nchini Uswisi akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Annan alikuwa ni mwafrika wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akitumikia mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Aidha baada ya kumaliza muda wake alibaki kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu ya amani ya mzozo wa nchi hiyo.
Hata hivyo, kipindi cha Annan akitumikia nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kilikuwa na na changamoto ya vita vya Iraq.