Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

Utenguzi wa Kemikimba, umetangazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus katika Taarifa yake aliyoitoa kwa Vyombo vysa Habari Agosti 18, 2023.

Kemikimba aliteuliwa kushika nafasi hiyo  Februari 26, 2023 na aliapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma Februari 27, 2023.

Awali Kemikimba aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kutumikia nafasi mbalimbali ikiwEmo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Maji.

Serikali yafunga Makanisa matano
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 19, 2023