Kiongozi wa Kituo cha Redio Gorilla FM ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Wanahabari wa Congo-UNPC huko Kivu Kusini, Egide Kitumaini ameshambuliwa na watu wenye silaha muda mfupi baada ya kurudi nyumbani kwake.

Akisimulia tukio hilo, Kitumaini amesema “watu wawili waliingia ndani nawengine wanne walibaki nje. Tulionana nao wala hawakuficha nyuso zao, mmoja kati yao alikuwa na silaha ya AK 47 mkononi sijui kwanini hakunifyatulia papo hapo alipoingia.”

Kiongozi wa Kituo cha Redio Gorilla FM ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Wanahabari wa Congo-UNPC Kivu Kusini, Egide Kitumaini.

Alisema, “hapo nilipambana nao hadi jikoni na hapo walifyatua risasi mara tatu, moja imenipita kati ya vidole. Mara watoto walipolalamika waliondoka haraka ila walichukua vifaa vyangu vya kazi. Lakini inaonekana kwamba mmoja aliumia kwa risasi kwani kuna damu njia yote waliopitia.”

Muungano wa wanahabari katika jimbo la Kivu kusini, umelaani shambulizi hilo ukisema ni kitendo cha kinyama na kuzitaka mamlaka kufuatilia sulala hilo pia kuhakikisha usalama wa Wanahabari wakati huu ambapo mchakato wa uchaguzi nchini Congo ukiendelea.

Young Africans kushusha wengine wanne
Mzee Chasamba atoboa siri Mwl. Nyerere alivyompa Ukamanda