Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, imetupilia mbali kesi iliyotaka kumzuia Mwanasiasa wa upinzani, Moise Katumbi kuwania urais kwa madai kuwa si raia wa Kongo.
Kesi hiyo, ambayo iliwasilishwa Mahakamani na mgombea mwingine wa kiti cha Urais, Noel Tshiani alidai kuwa Katiba ya Kongo hairuhusu uraia pacha kwa kuwa baba wa Katumbi alikuwa raia wa Italia.
Hata hivyo, Wakili wa Katumbi, Herve Diakiese alisema hakuna uthibitisho wowote ya kuwa mteja wake ana uraia mwingine zaidi ya ule wa Kongo na Tshiami hakuwa na uthibitisho mwingine hivyo Mahakama kufikia uamuzi huo.
Moise Katumbi (58), Mfanyabiashara na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombea wakuu dhidi ya Rais aliye madarakani, Felix Tshisekedi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 20, 2023.