Ajali ya gari dogo la kusafiria kuligonga Lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa Barabara kuu ya Mtwara – Lindi kutokana na hitilafu, imesababisha umauti wa watu watatu na wengine wanne kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mtaki Kurwijila amesema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Alphad lenye namba za usajili T404 EDB kuliigonga Lori hilo aina ya Howo lenye namba za usajili T 203 DKB na pikipiki ambayo namba zake hazijatambulika.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa Dereva wa Alphad iliyokuwa imebeba abiria saba, Yahya Juma (35), kushindwa kuchukua tahadhari barabarani ambaye pia alitoroka mara baada ya ajali hiyo iliyotokea Oktoba 29, 2023 majira ya saa 11:50 usiku, eneo la mlima wa soda Mikindani.

Kamanda Kurwijila amewataja waliofariki kuwa ni Mwanaidi Seleman Ahmad (51), Niale Ally (32) na Mohamed Mfaume Mtumanuma (60) wote Wakazi wa Mtwara, huku mashuhuda wakidai kuwa baada ya kuligonga Lori pia gari ikamgonga na Dereva pikipiki, Diocles Peter (25).

Katumbi ruksa kugombea urais DRC - Mahakama
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 31, 2023