Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa ufafanuzi wowote kuhusiana na suala la chanjo ya uviko 19 anautoa kanisa kwake.
Akizungumza na Dar24Media Askofu Gwajima amesema kanuni hazimruhusu kuongea na media kuhusiana na suala la chanjo ya uviko 19.
“Mimi siongei na media sijapata muda wa kuongea na media bado, kwaiyo siwezi kuongea na media mambo haya , sijaongea na media bado,” Amesema Askofu Gwajima.
Aidha alipoulizwa na Dar24Media kuhusiana na kauli ya agizo alilolitoa Waziri Gwajima kwa Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Askofu Gwajima amesema Kanuni hazimruhusu kuongea na media.
“Ukiona naongea ujue naongea na watu kanisani, nitawafafanulia watu wangu wa kanisani sio media, kanuni haziniruhusu kuongea na media,” Amesema Askofu Gwajima.
Hata hivyo Askofu Gwajima ameialika Dar24Media kanisa kwake Jumapili ya Agosti 22, 2021 baada ya kuulizwa kama wanaruhusiwa ndipo akasema mtu yoyote anaetaka kuja kanisani anaruhusiwa kwani kanisa ni wazi kwa kila mtu.
Katika hatua nyingine Leo Agosti 18, 2021 Waziri wa Afya, Maendeleo, ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima ametoa taarifa ya agizo alilolitoa hapo jana Agosti 17, 2021 kuhusiana na kukamatwa kwa Askofu Gwajima, wakati akikagua jengo la huduma za mama na mtoto katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure. Amesema kauli ya IGP Sirro ya kuomba barua ya mamlaka ni sahihi hivyo hana budi kuheshimu taarifa ya IGP sirro.
Wakati huo huo Dkt Doroth Gwajima, amewahasa wananchi kuacha tabia ya kutengeneza ajenda zao wenyewe kwa kupotosha kauli zinazozungumzwa na viongozi.