Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa mwongozo wa maadili ya Taifa kupitia kwa Mkurugenzi wa idara ya utamaduni Dkt. Emmanuel Temu.

Kupitia kikao kilichofanywa leo Jumatano Agosti 18 jijini Dodoma, akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya Utamaduni, Dkt Emmanuel Temu, ametanabaisha kuwa lengo la kikao ni kuboresha  Mwongozo wa Maadili ya Taifa na Utamaduni wa Mtanzania ili kulinusuru Taifa dhidi ya mmomonyoko wa Maadili na utamaduni wa nchi.

 â€śKitabu kinalenga kutoa mwongozo kwa jamii ya kitanzania kurejea katika misingi yetu ya maadili kama Taifa kwa kupenda, kuthamini na kuheshimu mila na desturi zetu ambazo ni miongoni mwa nguzo kuu za utamaduni wetu”. Amefafanua Dkt. Temu.

Aidha, amesema kitabu hicho cha Mwongozo kinazingatia Tamko la Sera ya Utamaduni la mwaka 1997, Sura ya Pili, Kipengele cha Pili, Sehemu ya Tatu (2:2:3) kuwa tuna wajibu wa kurithisha na kuendeleza Maadili, Mila, na Desturi Nzuri.

Hatahivyo kitabu hicho kinakusudia kutoa mwelekeo na umuhimu wa kuzingatia maadili kwa makundi mbalimbali ya jamii wakimemo wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu, vijana, watumishi wa umma na jamii kwa ujumla.

Akiwapitisha wajumbe katika yaliyomo ya kitabu hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni anayeshughulikia eneo la Lugha, Dkt. Resan Mnata amesema kitabu hicho kina na jumla ya sura tano, ambapo sura ya Kwanza imejikita katika Usuli; Sura ya Pili mmomonyoko wa maadili katika jamii; Sura tatu wajibu wa makundi mbali mbali katika kukuza na kuendeleza Utamaduni na maadili; Sura ya nne Usimamizi, uhifadhi, utekelezaji na uendelezaji wa utamaduni na maadili na Sura ya tano mambo muhimu ya kuzingatia na mapendekezo.

Wajumbe wengine walio changia ni Mjumbe kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bona Leon, Katibu Mkuu wa Habari Dkt. Hassan Abbasi na Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wameunga mkono suala hili na kusisitiza kutengenezwa katika Lugha rahisi pia kufundishwa katika ngazi mbalimbali za elimu.

Mwenge wa Uhuru kukagua miradi 46 Dar
Kauli ya Askofu Gwajima kwa Waziri