Machafuko yameibuka kwenye mji wa Jalalabad nchini Afghanistan baada ya wanamgambo wa Taliban kuanza kupandisha bendera yao ya Taifa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya Taliban kuchuka nafasi ya  aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Ashraf Ghani, wamekuwa wakiondoa bendera ya Taifa na kuweka bendera yao.

Hatua hiyo imesababisha machafuko katika mji wa kibiashara wa Jalalabad imeelezwa kuwa watu wengi hawafurahii suala hilo.  Kumekuwa na upinzani kuhusu suala hilo kwa sehemu kubwa ya jamii  ya Afghanistan,mitandao ya kijamii imeonesha picha na video za maandamano na watu wanaopeperusha bendera katika mitaa mbalimbali ya mji wa Jalalabad.

Aidha Taliban wameweka bendera  katika uwanja muhimu huko Jalalabad na kwamba kumekuwa na mapigano na watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa na vikosi hivyo.

Mpaka sasa watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine kumi na mbili wamejeruhiwa baada ya kupigwa risasi.

Dkt. Gwajima awakaba wanaume
Hali ya hewa Morocco yatibua mipango