Uongozi wa Klabu ya Chelsea ya England umesikitika baada ya Thomas Tuchel kukiri hadharani kwamba anavutiwa na kocha wa timu hiyo, Anthony Barry na angependa kufanya naye kazi baada ya kuajiriwa FC Bayern Munich mwishoni mwa juma lililopita.

Tuchel alikabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi FC Bayern Munich, baada ya kutimuliwa kwa Julian Nagelsmann, na ameanza kulisuka benchi lake la ufundi huku akimpeendekeza Barry katika mipango ya kuinoa timu hiyo, jambo ambalo limewakera mabosi wa Chelsea.

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani aliulizwa kuhusu mipango yake mbele ya waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba na Uongozi wa FC Bayern, Tuchel akaweka wazi anatamani amjumuishe Barry katika benchi lake la ufundi kutokana na uzoefu alionao, huku wengine waliotajwa ni Arno Arno Michels na Zsolt Low.

Tuchel alisema hao ni watu ambao amefanya nao kazi kwa muda mrefu na wanafahamu mbinu zake za ufundishaji.

“Bado sijaandaa benchi la ufundi, nimefurahi Arno Micheles na Zsolt Low watakuwepo, nimefanya nao kazi kwa muda wa miaka 10, matumaini yetu ni kumuongeza Anthony Barry ambaye yupo Chelsea,” amesema Tuchel.

Aidha Chelsea haijapendezwa na kitendo cha Tuchel kuzungumza maneno hayo hadharani tena mbele ya waandishi wa habari.

Barry bado ana mkataba Stamford Bridge na mara ya kwanza alijiunga akiwa chini ya Frank Lampard ambaye walisomea ukocha pamoja kutoka Wigan, Hiyo inamaanisha Bayern Munich italazimika kuilipa Chelsea fidia.

Baada ya Lampard kufukuzwa kazi Tuchel alichukua mikoba yake mwaka 2021 akaisaidia kubeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya msimu wake wa kwanza.

Barry, ni kocha mzoefu mwenye jina kubwa, elimu yake aliipata katika Chuo cha St George Park kabla ya kuungana na Tuchel katika benchi lake la ufundi, Barry aliwahi kuwa katika benchi la ufundi la kikosi cha Ubelgiji kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia.

Liverpool yamuwinda Antonio Silva
Robertinho afurahishwa na kiwango Simba SC