Klabu ya Chelsea inaonekana kupata hasara kubwa kwa Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye amezifumania nyavu mara tano pekee akiwa Inter Milan ya Italia kwa mkopo msimu huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Football Insider, The Blues’ wako tayari kumuuza Mshambuliaji huyo mwishoni mwa msimu huu, huku Inter ikiwa na uwezekano wa kujaribu kuongeza muda wa kuendelea kuwa naye.

Chelsea walitumia Pauni Milioni 97.5 kumrejesha Lukaku Stamford Bridge mnamo Agosti 2021 akitokea Inter Milan, lakini sasa kuna uwezekano wa kumuuza jumla.

Taarifa zinaeleza kuwa huenda Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wanajipanga kumsajili Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bayern inavutiwa na mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, ambaye ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani iwapo anakuwa fiti bila majeraha.

Hata hivyo, Bayern haitaanza mazungumzo na Chelsea hadi mwishoni mwa msimu huu.

Mabingwa hao wa Ujerumani walikuwa wakihusishwa na Harry Kane wakitafuta mtu wa kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski, ambaye aliondoka kwenda FC Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita.

Hata hivyo Chelsea wanaweza kujaribu kupata dili na AS Roma kwa kubadilishana mkataba unaomhusisha kinda Tammy. Abraham ambaye aliwahi kupita klabuni hapo.

Makamu wa Rais wa Marekani kuipaisha Tanzania Kimataifa
Simba SC kuifuata Raja Casablanca kwa mfungu