Kocha Mkuu wa Young Africans, Cedric Kaze ametaja mambo matano muhimu alioyafanya hivi karibuni baada ya kuvuna alama mbili katika michezo miwili mfululizo, ikifuatiwa na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa juma lililopita.

Kaze ameyataja mambo hayo ambayo yalimpa presha kubwa pamoja na kumnyima usingizi, kufautia maneno yaliyozungumzwa kuhusu kikosi chake kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijami.

“Yanga ni timu kubwa, hivyo kama kocha na ikizingatia ndio mgeni na kujua ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu Bara ilinifanya kuwa na presha kubwa, lakini nimebaini na nimefanyia kazi, tayari nimejua ligi ya hapa ikoje,” amesema.

Kitu kingine ni kuwa alibadilisha mfumo wa mazoezi na kuyafanya kuwa ya nguvu aliyoyaona matunda yake katika mchezo uliopita.

Kaze amesema alibaini pia wachezaji wana hofu kubwa wawapo uwanjani, hivyo alijitahidi kuwaondolea na kuwafanya wajiamini ili kupata matokeo na kufikia malengo ya kutwaa taji.

Jambo la nne ni kutengeneza muunganiko mzuri wa wachezaji wake ili kutofungwa kwa urahisi, ila alishangaa kuona safu ya ulinzi inaruhusu kufungwa kirahisi.

Akizungumzia la jambo la tano, amesema ni suala la morali ya wachezaji ambao amejitahidi kuijenga baada ya matokeo ya sare na walimuelewa na kufanyia kazi alichowataka kukifanya ambacho kimezaa matunda.

TPLB yarusha kijembe Misri
Barbara: Kazi ndio imeanza Simba SC