Aliyekuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (IBK), ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kulazwa hospitalini Jumanne wiki hii.
Familia yake imedai kuwa ulikuwa uchunguzi wa kawaida wa matibabu, lakini duru za hospitali zimebainisha kwamba alikuwa amepatwa na ugonjwa wa aina ya kiharusi.
Wakati huohuo ujumbe wa kundi la wanajeshi waliompindua madarakani ukiongozwa na kiongozi wake Kanali Assimi Goïta, ulikwenda kumuona hospitalini na kumtakia heri aweze kupona haraka.
Kulingana na vyanzo vya hospitali Keita aliyekuwa amelazwa kwa siku mbili katika hospitali ya Pasteur mjini Bamako alirudi nyumbani jana alhamisi jioni baada ya kuonekana kuwa na hali nzuri.