Klabu ya Simba SC imetambulisha rasmi Kocha wa Viungo Kelvin Mandla kutoka nchini Afrika Kusini, ambaye anajiunga na Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.
Simba SC imekua ikipitia wakati mgumu baada ya kuondoka kwa Kocha wa Viungo Sbai Karim aliyeongozana na aliyekua Kocha wa Klabu hiyo kutoka Serbia Zoran Maki ambaye aliyeamua kutimka mwanzoni mwa msimu huu, ikiwa ni siku chache baada ya kusaini mkataba wa kuanza kazi klabuni hapo.
Kocha Mandla ametangazwa kupitia Simba App na Kurasa za Mitandao za Klabu ya Simba leo Alhamis (Novemba 17), majira ya saa kumi jioni, akitanguliwa na Kocha wa Makipa Chlouha Zakaria, ambaye aliyetambulishwa mwanzoni mwa juma hili.
Kutambulishwa wa Kocha huyo kunatarajiwa mabadiliko makubwa katika utimamu wa miili ya Wachezaji wa Simba SC ambao wamekua wakilalamikiwa kukosa sifa ya kuhimili upinzani kutoka kwenye timu pinzani wanazokutana nazo katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.
Simba SC Jumamosi itacheza dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, katika muendelezo wa kuzisaka alama tatu za Ligi Kuu msimu huu 2022/23.
Jana Jumatano (Novemba 16), Simba SC ilicheza dhidi ya Namungo FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi wa 1-0, bao likifungwa na MShambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri.