Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo amewatahadharisha Waandishi wa Habari juu ya suala la kujikita na uandikaji wa habari za matukio na kuziacha zile zenye utafiti kwani Uandishi wa habari za matukio hauna tija kwa Taifa na hauleti maendeleo yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Mallimbo ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo kwa waandishi wa habari, kutoka mikoa Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa and Ruvuma, na kuyataja maeneo mengine yenye changamoto katika uandishi kuwa ni kukosekana kwa chanzo ambacho kinampa uhalali mwandishi kuandikia Habari.

Amesema, kukosekana kwa mitazamo tofauti kutoka kwa watoa habari na kushindwa kutafsiri takwimu katika muktadha ambao mwananchi ataelewa pia unachangia katika kuleta mkanganyiko na hivyo kufanya kukosekata kwa utafiti wa kutosha wa habari yenyewe.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (Office of High Commissioner for Human Rights, East Africa Region Office (OHCHR-EARO), Catherine Njuguna, akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu kazi zinazofanywa na (OHCHR-EARO), jijini Mbeya.

Mafunzo hayo, ambayo yanadhaminiwa na Kamishna wa Haki za Binadamu Ofisi ya Afrika Mashariki (OHCHR-EARO), yanafanyika katika jiji la Mbeya kwa siku tatu, na ni mafunzo ambayo hufanyika sambamba na Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (MCT).

Aidha, pia yanalenga kuwaongezea ujuzi waandishi wa habari kuandika habari zinazoweza kushindana ndani na nje ya nchi na kuondokana na uandishi wa matukio na badala yake wajikite kwenye uandishi wenye uchambuzi ili kuleta tija kwa jamii.

Hii ni mara ya pili Baraza kuendesha mafunzo hayo, ambapo awali mwezi Agosti, 2022 yalifanyika mkoani Mtwara, na yanatarajia kufanyika tena jijini Arusha mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu (2022).

Rais Samia apewa Tuzo ya Heshima amani na utulivu
Kelvin Mandla amrithi Sbai Karim Simba SC