Jumuiya ya Maridhiano Tanzania imekabidhi Tuzo ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutokana na kuendelea kuimarisha hali ya amani na utulivu nchini.

Tuzo hiyo, imepokelewa jijini Mbeya kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera.

Tuzo iliyotolewa kwa Rais Samia.

Akipokea tuzo hiyo, Homera amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri, afya pamoja na miradi ya maji mkoani humo.

Aidha, viongozi wa Dini wa mkoa wa Mbeya wamefanya maombi maalum kuliombea Taifa amani na mvua na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais.

Ndege ATCL yashindwa kutua uwanja wa Bukoba
Uandishi bila tafiti: Wanahabari waonywa