Wakili wa timu ya wanasheria wa kiongozi wa Azimio, Raila Odinga, Julie Soweto ametoa wasilisho la moja kwa moja la video ili kuonyesha hitilafu kutoka kwa tovuti ya Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC ikionesha raiwa wa kigeni aliyepiga kura ya urais wakati wa uchaguzi.
Wakati wa kusikilizwa kwa ombi la Mahakama ya Juu katika uchaguzi wa urais, alitoa fomu kutoka Shule ya Msingi ya Gacharaigo katika Kaunti ya Murang’a iliyokuwa na jina la raia wa Venezuela Jose Camargo.
Amesema, “Kutoka nilipo, muhuri wa IEBC unaonekana umebandikwa juu juu ya muhuri mwingine na tumeombwa tuoneshe jinsi takwimu zinavyobadilika sasa tukiangalia kura zilizopigwa.”
Bi. Soweto ameongeza kuwa,”Katika fomu hii nambari ya kwanza ni ya Raila Odinga mwenye kura 55, Ruto 260, Mwaure 1 na Wajackoyah 0 na tukijumlisha jumla ya kura tunapata 316, jumla ya kura zilizopigwa kulingana na fomu hii ni 321 hii ina maana kwamba ukikokotoa utapata jawabu lenye tatizo.”
Amefafanua kuwa, “Tuliambiwa na Eric Gumbo (wakili wa IEBC) kwamba hakukuwa na wageni katika uchaguzi huu, na tuliambiwa hawakupata seva katika kona ya juu kushoto tuna jina la Jose Camargo na huyu ndiye mtu ambaye kuamua matokeo ya uchaguzi. Je, hilo lilikujaje huko?.”
Hata hivyo, Bi Soweto ameongeza kuwa raia huyo wa nje, Carmago alikuwa akiingilia Fomu za 34As za tume ya IEBC na kusema ushahidi huo unaonesha ni jinsi gani kuna matatizo mengi wakati wa zoezi la upigaji kura hadi kutolewa kwa matokeo hayo.