Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa mahakama nchini humo ina matatizo makubwa hivyo amesema kuwa inahitaji kufanyiwa marekebisho ambayo yatakuwa msaada mkubwa wananchi.
Ameyasema hayo mara baada ya mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni na kuibuka mshindi wa nafasi ya kiti cha uraisi wa nchi hiyo kitu ambacho kilipingwa vikali na mpinzani wake Raila Odinga.
Kenyatta amesema kuwa mahakama nchini humo inahitaji marekebisho makubwa hivyo ameongeza kuwa maamuzi yeyote yatakayoamuliwa na mahakama hiyo atayaheshimu na kuyaunga mkono.
”Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali, sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari,”amesema Kenyatta.
Hata hivyo, Rais huyo ameonekana kuwa na hasira na majaji wa mahakama kuu nchini humo baada ya kutenguliwa kwa matokeo hayo ambayo yalimpa ushindi wa kiti cha urais wa ncvhi hiyo.