Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewasili nchini Cuba kuanza ziara yake rasmi ya siku tatu. Kupitia taarifa ya msemaji wa ikulu ya Kenya, Manoah Esipisu, amesema kuwa ziara hiyo itaangazia masuala ya Afya, biashara na utamaduni.
Amesema kuwa Kenya inatathmini mfumo wa afya wa Cuba katika juhudi za kuimarisha sekta yake katika nyanja hiyo, ambayo ni moja ya nguzo nne muhimu zinazoangaziwa na utawala wa Kenyatta katika muhula wake wa pili madarakani.
Cuba ina mfumo wa afya unaosifika duniani kote.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, kila daktari mmoja anahudumia watu 150 nchini Cuba, ikilinganishwa na Kenya, ambako kila watu 16,000 wanahudumiwa na daktari mmoja.
-
Rapa Rick Ross Kutumbuiza Nchini Kenya
-
Prof. Tibaijuka awachana viongozi wa serikali ya awamu ya tano
-
Serikali yalivalia njuga tatizo la nguvu za kiume
Kenyattta anatarajiwa kukutana na rais Raul Castrol na vile vile kufungua rasmi ubalozi wa Kenya nchini Cuba. Ubalozi wa Kenya nchini Cuba ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2016.