Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Morris International kilichopo mkoani Morogoro.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli ametembelea kiwanda hicho na kushuhudia namna sigara zinavyotengenezwa kuanzia katika hatua ya kwanza mpaka sigara inapokamilika kwa matumizi au kwa ajili ya kuuzwa.

Kwa upande wake Mmiliki wa kiwanda hicho amesema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho kimeajiri zaidi ya watu mia mbili na ishirini na nne ambao wanahusika katika kuhakikisha uzalishaji unakwenda salama.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuzalisha ajira kwa wingi kwa Watanzania.

 

Kenyatta kukutana na rais Castro nchini Cuba
Michael Richard Wambura atupwa jela maisha